
Basi mida ya jioni Mike na Mama yake walikaa mezani. Chakula kililetwa, Ciara hakuonesha hofu usoni mwake ukilinganisha na Watumwa wengine. "Karibuni chakula...." Ciara aliongea Vile Katy alikuwa na shauku ya kutoa adhabu endapo chakula kitakuwa kibaya aliwahi kushika kijiko. Kadri alivyozidi kula ndivyo hasira na kisirani viliyeyuka. "Hiki chakula kapika nani siamini kama kimepikwa na watu wengi" Katy aliuliza "Kapika Katy....." Jala (Mtumwa mwenye umri mkubwa kuliko wote) alizungumza Umepika vizuri kama unampikia Mama yako, na hivyo ndivyo inatakiwa kuwa bila kujalisha nyie ni Watumwa mahali hapa" Katy aliongea Muda wote macho ya Mike yalikuwa kwa Ciara, ni vile
0 Comments