
Nilichanganyikiwa—ameniibia? Yeye ana nguo nzuri, mbona anachukua zangu? Nikampigia, nikasema, “Neema, nguo zangu ziko wapi?” Akasema, “Una nguo wewe?” Nikasema, “Neema, sio utani, nimeoga, nataka kuvaa!” Akasema, “Magwanda yako nimeyachukua, tulia, nakuja.” Nikasema, “Unamaanisha nini?” Akasema, “Tulia, nakuja sasa!” Akakata simu. Nilishangaa, lakini nikatulia. Baada ya nusu saa, alirudi na begi la nguo. Akasema, “Hizi ndizo nguo, chukua.” Nikasema, “Nguo gani hizi? Zangu ziko wapi?” Akasema, “Zile nimewagawia watu, hizi nimenunua, za mtumba, bei nafuu, zitakufaa.” Akanivua kitenge, nikabaki uchi, nikasema, “Neema, nini sasa?” Akasema, “Shoga, umeumbika! Hata mimi ninakutamani!” Nikasema, “Toka, niache!” Akasema, “Tuliambiwa nini unyagoni kuhusu vichaka?” Nikacheka.
0 Comments