
"Malipo?.... nadhani hutudai ..." Secretary Annie aliongea huku akipitia kumbukumbu zote za malipo chapu chapu. "Oh nadhani nimesahau kwanini nilikuwa hapa " Tasha alibeba pochi yake kisha akaondoka ilihali machozi yana mlenga lenga. Secretary Annie aliachia kicheko cha chini chini. "Inaonekana Tasha alikuwa anamtaka sana Bryant Kobe sasa kaondoka bila kumuaga ni aibu tupu katika moyo wake. Natarajia kuona somo Tiktok very soon kuhusu hiki kitukio " Alizidi kujichekesha, ile anainua kichwa chake alikutana na macho ya Philips Kobe yakiwa yamekaza. "Unajua ukimfuatilia Tasha mtandaoni utagundua ni binti ambaye hababaishwi na Wanaume, yaani kuna wakati utahisi yeye ndio anaoa....kanifurahisha sana
0 Comments