
" Tayari unaweza kwenda Sasa Yani unaonekana handsome kama kawaida yako " " Usifanye kitu chochote bila kuambiwa wakati mwingine " aliongea Elian kwa amri " Sawa mkuu nimekupata ,ila usisahau ahadi yako " alisema Winnie ,Elian alitingisha kichwa akaondoka Kwa upande wa Levis akiwa chumbani kwake " Mr Charles kile chumba Cha pembeni ya chumba Cha Dad Kuna mgeni ?" Levis alimuuliza mr Charles " Ndiyo Kuna mgeni amefika Leo pia " alijibu Mr Charles huku anapanga nguo za Levis kabatini "Ni nani huyo mgeni na jina lake ni nani na ana uhusiano gani na Dad?" Levis aliuliza maswali
0 Comments