
mwanaume kichaa nje ya jumba langu akiwa ameketi na makorokoro yake, siku ya kwanza niliogopa kidogo kwani alilala hapo na makorokoro yake mpaka kukakucha, siku ya pili pia alifanya hivyo lakini siku ya tatu nilianza kumuhisi vibaya maana vichaa wengi wamekuwa wakitumiwa na majambazi katika kazi zao atakuja karibu na nyumba yako atapiga kambi wewe utajua ni kichaa kumbe ni msoma ramani. Basi nikataka kwenda kunfukuza lakini roho yangu ilisita kwa woga kwani sura yake ilikuwa inatisha vibaya mno, rundo la nywele chafu lilijikusanya kichwani mwake na isitoshe alikuwa anavuta mamisokoto sijui ni bangi au ni gonzo mwenzenu nikajihami hata
0 Comments