
na rafiki yake aitwae Tausi, "Leo kazi ipo" sauti nzito ilipita kwenye masikio ya Kayoza na kushindwa kuelewa inatokea wapi, na cha ajabu sio Denis wala Omary aliyeweza kuisikia sauti hiyo.... _________________ MUENDELEZO _________________ "Jamani hamsikii sauti yoyote ya kutisha?" kayoza aliwauliza wenzake baada ya kuwaona kama hawasikii anachokisikia yeye, "Sauti gani?" Denis aliuliza, "Sauti nzito inakwaruza masikioni" Kayoza alijibu na wenzake wakaishia kucheka, "Acha mawenge wewe, au unapata uoga kukutana na Stellah?" Omary aliongea huku akimcheka kayoza, "Acha ujinga, mimi sijamuongelea Stellah hapa, naongelea ishu nyingine" Kayoza aliongea baada ya kutofurahishwa na maneno ya Omary, "Yaishe basi, kifupi sisi
0 Comments