
SEHEMU YA 1 Leila ni binti wa miaka 22 tu, lakini majukumu aliyobeba kichwani yanazidi hata mzee wa miaka 40. Kila mtu kwao alimtegemea yeye😫. Alikuwa anaishi na mama yake Bi Salma, mdogo wake wa kike Lulu mwenye matatizo ya figo, na mdogo wa kiume Leo ambaye bado alikuwa yupo darasa la nne. Baba yao alishafariki muda mrefu, na tokea hapo maisha yakaanza kubana mno💔. Kila asubuhi Leila aliamka mapema kwenda kuchanja madafu kwenye mkokoteni wake pale Coco Beach. Ni biashara aliyo amua kuifanya baada ya kuhangaika sana kutafuta kazi. Pesa yake aliyo pata iligawanyika mara tatu, alinunua dawa za
0 Comments