
"Machoni Mwangu Kuna Jibu" 🌙 Usiku huo haukuwa wa kawaida kwa Zainabu. Alikuwa amekaa juu ya dari ya ghorofa ya pili ya hosteli yao, akitazama anga lililojaa nyota. Kilio cha ndani kilikuwa kimya, lakini macho yake yaliwasema yote. Alikuwa amechoka na kubeba hisia ambazo hazina jibu, moyo wake ukimuita mtu mmoja tu — Ayoub. Ayoub alikuwa kijana mnyenyekevu, mwenye akili, mwenye ndoto kubwa, lakini pia mwenye ukimya wa kuumiza. Aliongea kwa macho zaidi ya mdomo, na kila alipomtazama Zainabu, kulikuwa na kitu ambacho hakijawahi kusemwa. Zainabu alijiuliza tena na tena, "Hivi ananipenda au ananionea huruma tu?" Kila mara Ayoub alipokuwa
0 Comments