
MWANZO....... Naongelea kipindi dunia haijachangamka, ni kile kipindi usafiri wetu ulikuwa ni farasi, mikuki na mishale pamoja na upanga ndio zilikuwa silaha zetu. "Kibao kabisa kinajieleza ni marufuku kukojoa kwenye hili eneo faini ni vipande saba vya dhahabu, wewe haugopi" Nilishtuliwa na sauti ya kiume, kojo ndio kwanza lilikuwa linamwagika isingekuwa rahisi kujizuia kama ni kukamatwa acha iwe hivyo tu. Baada ya kumaliza nilisimama, si unajua tena ukojoaji wetu wa kuibia huwa hatuvui chupi yote badala yake huwa tunaisogeza pembeni tu 😄. "Ulikuwa unasemaje?" Nilijitia mkali na huku kosa ni la kwangu. "Kusemaje nini! hili bango limeandikwa nini?" "Sijui hata
0 Comments