
( Ni sauti ya mama wa kambo aliyeolewa na baba siku Saba kuisha anaonyesha kucha zake mapema nikaenda kumsikiliza) " Nam mama shikamoo kwanza. " Sitaki shikamoo yako nimekuita hapa kukwambia wewe una umli wa miaka 16 mdogo wako miaka 10 na uyu mwengine miaka 7...kuanzia Leo wewe ndio utakuwa msonga ugali humu ndani na isitoshe usikae kizembe ata pesa ukatafute uwasaidie wadogo zako. ( Hapo kwenye kutafuta pesa ndio kipengere ila kupika ata yeye kabla ajaja si nilikuwa nawapikia wadogo zangu Nikamwambia) " Mama mimi bado nasoma sasa ivi swala la kazi nitakuja kufanya ila kupika ilo lisikuumize kichwa
0 Comments