
PART 7: MTI UNAOMWAGIKA DAMU Maelezo ya yule bibi kikongwe ilizidi kuwaacha midomo wazi wanakijiji. Wengine wakawa wanakumbuka hadithi walizosimuliwa na wazee wao zamani. Inafanania na haya wanayoyaona Sasa. Kumbe haizikuwa hadithi bali ni kweli. "Ndiomana watoto wetu wanaumwa sana hapa kijijini" Alisema mama Janeth "Ndiomana tunasikia sauti za ajabu usiku" Bwana Zengo alisema Kila mmoja alikuwa anasema lake kulingana na maelezo ya yule bibi kikongwe. Ghafla upepo mkali ukavuma wakiwa pale kwenye mti wakishangaa mafuvu. Ule mti ukaanza kujikunja kama mtu hai. Damu ikazidi na kuzidi. Nyufa kubwa zikaanza kutokea ardhini, ardhi ilianza kujiachia. Mafuvu mengi yakaanza kunyoosha mikono
0 Comments