
PART 8: MTI UNAOMWAGIKA DAMU Siku iliyofuata, wanakijiji wote walikusanyika tena kwenye ule mti. Walikaa kwa kuuzunguka. Damu iliendelea kutiririka taratibu. Yale mafuvu walioyafukua waliyahifadhi kwenye chungu kikubwa cha udongo wa mfinyanzi na kuifunika vitambaa vyeupe. Mganga wakijiji alitembea taratibu akiwa na ungo uliojaa dhana zake za kazi. Alikuwa amevalia shuka jeupe. Wanakijiji walikaa kimya wakisubiri kuona kitakacho tokea. "Leo ni siku ya kuweka ukweli wazi" Alisema Mganga na kuendelea baada ya kunyamaza kidogo "Siku ya kuomba msamaha" Alisema, alichukua pembe yake kubwa na kuupuliza. Alipuliza kwa dakika zisizozidi mbili kisha akaagiza aletewe mbuzi mweupe haraka. Alipoletewa akamkata kichwa na
0 Comments