
Leo nataka niwape hadithi ya maisha yangu, hadithi ambayo mtanitumia mimi kama mfano na kuishi mazuri yangu na kuachana na mabaya yangu ambayo nitakuwa nimeyafanya katika maisha yangu. Jina langu ni Rodrick, mimi naitwa Rodrick. Sitaki kukuzungusha sana, nitaenda moja kwa moja na mengine tutajua hapahapa nitajitahidi sana uelewe kila kitu. Nataka tu nianzie pale maisha yangu yalipoanza kuonesha upande wa pili wa dunia yangu. Na hapa ndiyo niliamini kuwa hakuna kitu hutokea bahati mbaya kwa maisha ya mwanadamu, kila kitu kina sababu, iwe nzuri au mbaya lakini tayari ni sababu na sababu hiyo itakupeleka mahali. Na hii ndiyo ilinitokea
0 Comments