
Niliendelea kumsaili huku moyoni nikisema “ni mwanamke anayevutia sana, amenivutia, ni mzuri sana.” Sijui hata kama unanielewa, nimetoka kanisani na kwa Mara ya kwanza naona kabisa nimekutana na love of my life (LOML). Sijamaliza hata kumtazama huyu mwanamke dereva naye alikuwa anaondoa gari. Nilikuwa hata nainamia, nataka kumuona yule mwanamke mzuri. Lakini nashindwa, nilichukia, nilitamani tu nishuke ila nawezaje. Sasa hapo G ananiambia “Mine Ricky, upo ok?” Nilimtazama, sio kwamba Gabriella ni mbaya, ana uzuri wake na si unajua mwenye pesa anajitunza vizuri ni mwanamke fulani hivi wa hadhi. Yule mwanamke ukimuona unajiuliza nimfuate au basi achana naye. Ni mzuri
0 Comments