
Yeye ndiyo mpenzi wa maisha yangu. Siku ya ndoa yangu ndiyo namuona mwanamke wa maisha yangu. Unaweza kucheka hata, wewe nicheke tu ila hapa sasa nipo na mke wangu kila nikimkukumbuka yule binti ndiyo nachanganyikiwa, natabasamu ovyoovyo akili yote kwake. Mpaka tunapiga picha akili yangu haipo kusema kweli, muda wa ukumbini umefika mimi hapa moyoni kwangu na akilini kwangu nawaza kuhusu mtoto mzuri niliyemuona kanisani. Kitu pekee nakumbuka ni tabasamu lake, na macho yake ni kama alikuwa ananitazama mimi vile hata nikawa natabasamu tu kijana wa watu. Rodricky mimi nilikuwa nimechanganyikiwa. Gabriella kadri anavyo deka mwilini mwangu, namna ananisogelea naona
0 Comments