
:01 Tangu nikiwa mdogo, kijana mdogo kabisa nimezoea kumuona mama yangu na bibi yangu tu. Nimekuwa nikiwa kwenye mazingira haya. Ni hawa watu wawili ambao mimi binafsi ninawapenda sana, ninawapenda kuliko kitu chochote kile. Mama yangu ni mama mpole sana, mama ambaye muda mwingi macho yake yamejaa maumivu, mama ambaye muda mwingi ni kama hana furaha kabisa. Hii hata kwenye ukuaji wangu imenisumbua. Ninakumbuka nyakati nyingine nilipokuwa nikitoka shule na kumkuta yeye nyumbani, nilimuuliza kwa upole “mama ulikuwa unalia?” Basi mama yangu alinitazama na kusema “hapana kijana wangu, kwanini nilie, kwanini mwanangu sijalia haya niambie kwanini na wewe unaonekana hivyo,
0 Comments