
Nikatokwa machozi nikisema “baba!!, baba yangu.” Aliniambia kwa hofu “tangulia tunapokutanaga, nakuja sasa hivi. Relax baby. Relax mpenzi wangu.” Sikuwa naweza hata kurelax, sikuweza hata kumjibu. Hata simu yangu niliacha palepale na kuanza kukimbia kuelekea mahali tunapobadili nguo. Ilikuwa hivyo, nilipofika katika chumba hicho nilikuta Joan pia anabadilisha nguo. Namna muonekano wangu ulivyokuwa, aliponiona alipata hofu. Joan aliniuliza “Kuna kini kwani Ndeana, mbona mara hivyo.” Nilmtazama tu, nikawa nabadili nguo nikisema “dada amesema baba yangu anaumwa sana.” Joan aliniambia “basi kwakuwa na mimi ndiyo natoka basi naomba tuongozane nikusindikize huonekani kuwa sawa.” Nilimtazama na kusema “Asante kipenzi ila wacha niende
0 Comments