
Siku zilizidi kusonga maisha yalibadilika kwa Dala alikuwa anavaa anapendeza na alisimamia kila kitu kuhusu Shalon pia alikuwa anaongozaba na dereva kumpeleka shalon shule pia kurudi dala alienda kumchukua. Walimu na wanafunzi walijua dala ndio mama mzazi wa shalon . Siku moja Dala alikuwa hajisikii vizuri ilimbidi Max aende kumchukua shalon shuleni . Kwakuwa alikuwa amechelewa kwenda shuleni alikuta wanafunzi wote wameondoka shalon alikuwa amekaa bustanini na mwalimu wake. Max aliwafuata na kusalimiana na mwalimu . " Baba shalon hongera sana kwa malezi ya binti yako. " Asante. Alijibu max huku akiwa anatabasamu lakini hakujua hiyo hongera inatokana na nini.
0 Comments