
Yaani mwenzenu hata ile meme inatembeaga kwamba ukitekwa mpenzi wako akikutafuta ndiyo umeokolewa mimi mwenzenu mnitoe huko. Maana nitatekwa kwa sekunde. Akiwa busy sana nusu saa. Stewart hajawahi kuwa ametingwa kwangu na ikiwa hivyo ananiambia na namuelewa. Hivyo nami nilimjibu “Am sorry jamani. Mr Tarick hajapeperusha njiwa wako. Nilichoka sana nikajilaza bahati mbaya ndiyo nashtuka hapq. Pumzika kesho mapema nitakuja kukuona.” Hapohapo akajibu “totoo usifanye hivyo tena kamwe, usifanye hivyo mimi utaniua nakuambia utaniua.” Nikacheka na kujibu “ndiyo unitumie meseji zote hizi na simu kunipigia kama unanidai figo.” Akaniambia “muone huyu, nakudai penzi Ndeana kwanza huwezi amini nimekumiss eti, kwani
0 Comments