
"Siwezi kufungua simu yangu na kwanini nifanye vile mnavyotaka nyie ?acheni kupoteza muda kwangu hamtopata chochote " Winnie aligoma kufungua simu yake " Kweli wewe ni mrembo na jasiri sana ndomana Mr Elian alikupenda kirahisi ,tunaweza kukuumiza wewe pamoja na mtoto wako kama hautatoa ushirikiano " alisema zero Winnie alianza kuogopa alishika tumbo lake " Tafadhali nawaomba msije mkajaribu kumuumiza mtoto wangu " Winnie aliongea huku analia " Kama hutaki iwe hivyo basi Fanya kila kitu tunachokwambia ,fungua simu yako na umpigie mr Elian " alisema zero Winnie alifanya kama alivyoelekezwa " Lete hiyo simu " vuvuzela alimnyanganya Winnie simu
0 Comments