
ukiweka orodha ya waimbaji bora wa nyimbo katika filamu za kihindi, ukaja kumwacha huyu utakuwa umefanya kosa la jinai. Anaitwa Abbas Kumar Ganguly akaja kutambulika kama Kishore Kumar. Mdogo wa gwiji wa maigizo Ashok Kumar anayetajwa ni moja ya waigizaji bora kuwahi kutokea India. Kishore Kumar alizaliwa mwaka 1929 akiwa ni wa mwisho katika familia yao. Wakubwa wake wakiwa ni Ashok Kumar, Sati Devi ambaye ni mke wa Sashadhar Mukherjee (huyu ni bibi yao mzaa baba kina Kajol na ndugu zake), pia kuna Anoop Kumar ambaye ni mwigizaji. Kishore alifuata nyayo za kaka zake Ashok na Anoop ila uigizaji haukuwa
0 Comments