
naenda kulala sababu siku hiyo nilikuwa na uchovu sana,nilionyeshwa chumba ambacho kilikuwa kwaajili yangu,niliingia ndani huku nikikiangalia chumba kwa umakini mkubwa sio siri kilikuwa chumba kizuri sana kwani kilikuwa na kitanda cha sita kwa sita,tv na vitu vingi vya kupendezesha Nilikaa kitandani na kuanza kuvua nguo ili nikaoge nitoe uchovu ndio nilale,wakati navua nguo nilishangaa mlango wangu ukigongwa taratibu,nilibaki najiuliza nani anagonga mlango lakini sikuwa na majibu,ilinibidi niamke taratibu nikafungue mlango nijue nani anagonga. SONGA NAYO Nilifungua mlango taratibu ili niangalie nani alikuwa anagonga,macho yangu yalikutana na mjomba akiwa ameshika dawa ya meno, mswaki na mazaga zaga mengine.Nilivipokea kisha nikarudi
0 Comments