
huku nikiwa naishangaa nyumba hile jinsi ilivyokuwa nzuri,ghafla walitoka ndani wasichana wawili ambao wakiwa na sura za tabasamu wakaenda kumkumbatia mjomba na shangazi Niliwaangalia watoto wale na kugundua kwamba walikuwa watoto wa mjomba kwani walifanana sana na shangazi,mmoja alikuwa mrefu kuliko mwenzake japo sio sana kwani walikuwa wanakaribiana,walipomaliza kusalimiana wakanigeukia na kunisalimia huku wakinishika mkono. SONGA NAYO Niliwashika mkono kwa zamu huku nikifurahia kushikana mikono na watoto wale kwani walikuwa wazuri kupindukia,kule kwetu kijijini hakuna hata msichana mmoja ambaye angeweza hata kidogo kufanana nao,tulipomaliza kusalimiana wakanipokea mizigo na kuanza kuelekea ndani. Tulipofika ndani nilikaribishwa sebuleni nilikuwa bado nashangaa shangaa kwani
0 Comments