
Baada ya kuondoka kwa kina Rasma pale nyumbani, nyumba ilitulia kidogo, vurugu zilipotea kabisa. Walibaki watu wawili tu—Mama na mtoto wake—wakiwa sebuleni, kila mmoja akimtazama mwenzake 👀. Garma hakuwahi kufikiria kwamba kumpoteza Mayner kungekuwa na athari kubwa kiasi hicho, lakini alihisi ametimiza wajibu wake. Kwake, hakupenda kudharauliwa. Kitendo cha Mayner kwenda kwa mganga, ilhali tayari alikuwa amemkataza, kilimvunja moyo na kumvunjia heshima 😤. Kama mwanaume, alihisi inampasa kuonyesha kuwa yeye ni nani. Mama yake alimtazama kwa sekunde kadhaa, kisha akasogea hadi alipokuwa na kusema: "Usijali, kila kitu kitaenda sawa. Yule hakuwa mwanamke wa maana wa kusema unataka kumuo..." Kabla hajamalizia,
0 Comments