
Walikula hadi walipomaliza, kisha Rasma alienda kuoga. Alipomaliza, alijiweka sawa kisha akaondoka huku akimuacha Mayner nyumbani. Upweke ulikuwa kwa Mayner. Aliendelea kuwaza kuhusu maisha yake mapya. Nyumba ya Rasma haikuwa kubwa, ilikuwa ndogo yenye vyumba viwili na sebule. Ingawa vyumba havikuwa vikubwa, lakini alikuwa na sehemu ya kujivunia na alikuwa analipa kodi kwa serikali. Akiwa kitandani, aliendelea kuchezea simu yake huku akijaribu kufuta picha alizopiga na Garma. Ilikuwa ngumu kwake kufuta baadhi ya picha 😢 lakini maneno ya mwanasaikolojia yalijirudia kichwani mwake. Alijikuta akifuta kila picha. Kuna muda chozi lilimdondokea kwenye kioo cha simu 😭. Alilifuta, lakini bado haikupunguza maumivu
0 Comments