
Laila alitamani kupokea simu ya rafiki yake lakini mkwara aliokuwa amepewa ulizidi kumuumiza kichwa. 🤯 Alijikuta akidondosha chozi. 😢 Moyo wake ulimuuma kuona mtu aliyemwahidi kila siku jana kushindwa kumsaidia. "Kama ameweza kumpa mtoto wake uchizi, atanishindwa mimi kweli?" 🤔 alijiuliza moyoni. Siku hii kwake ilikuwa kati ya siku ngumu zaidi kuwahi kumpata. 😔 Alikabiliwa na maamuzi mazito ambayo hakutegemea kuyachukua. Urafiki wake na Mayner ulikuwa mkubwa mno. Tangu utotoni walipocheza pamoja hadi ukubwani, ni hali ya kipato tu iliyowatenganisha, lakini siyo upendo. ❤️ Wakati mwingine Laila alikosa msaada kabisa, lakini kila alipomwendea Mayner na kumweleza, alimsaidia – hata kuongeza
0 Comments