
Bryan alipigiwa na usingizi akiwa amekaa, Maria aliendelea kuuchapa usingizi mpaka kulipokucha, alifumbua macho akajikuta kalala kwenye mapaja ya Bryan Tena akiwa kafunikwa vizuri na Bryan alikuwa bado kalala. Maria alijijnyanyua taratibu kutoka kwenye mapaja ya Bryan akakaa na kumuangalia usoni akiwa bado kafumba macho. " Kweli Ni kijana anaevutia Sana hawezi kukataliwa na mwanamke yoyote yule atakayemueleza anampenda lakini Mimi sio wa hadhi yake, siendani nae kabisa. Bryan alijitingisha Kama anataka kuamka, Maria alinyanyuka haraka akatoka nje akanjinyoosha viungo vya mwili wake na kuangalia juu. Jua ndio kwanza lilikuwa kinachomoza na ndege walikuwa wanaruka angani na wengine walikuwa wakiruka
0 Comments