BARUA YA HABARI ZA KIFO CHA ABU BAKR (R.A) KUTOKA MADINA NA KUPOKELEWA NA KHAALID BIN WALID KATIKATI YA VITA VYA YARMUUK

BARUA YA HABARI ZA KIFO CHA ABU BAKR (R.A) KUTOKA MADINA NA KUPOKELEWA NA KHAALID BIN WALID KATIKATI YA VITA VYA YARMUUK

Wakati wa vita vikubwa vya Yarmuuk, ambavyo vilikuwa chini ya uongozi wa shujaa wa Kiislamu na bingwa wa mbinu za kivita, Khaalid bin Walid (r.a), kulitokea tukio muhimu sana katika historia ya Uislamu. Katikati ya mapambano makali, alifika mjumbe kutoka Madina akiwa na barua kutoka kwa Khalifa mpya, Sayyiduna Umar bin Khattab (r.a). Barua hiyo ilikuwa na taarifa nzito kuhusu kufariki kwa Khalifa wa kwanza wa Waislamu, Abu Bakr as-Swiddiq (r.a). Khaalid bin Walid aliipokea barua ile akiwa kwenye mstari wa mbele wa vita. Alipoifungua na kuisoma kwa haraka, alikuta imeandikwa kwamba: Abu Bakr (r.a) amefariki na tayari amezikwa Madina.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments