
Masha alijichekesha tu mbele ya Mr Alberto lakini moyoni hakumtaka hata kidogo Rahul na hapo alipo kuja kumkatishia ndo kabisa akamuona mkosi kwakee ,"Mr Alberto ni zaidi ya mwanaume asante mungu umenipa huyu mwanaume jamani aaaah, najisikia hamu ya kumuona tenaaaa embu ngoja nimpigie ooh mungu wangu nimesahau hata kumuomba namba yake ya Tanzania hii haipatikani ,lakini si anakuja nyumbani mbona nina presha isiyo kuwa na maana?? Hahaha ooh jamani nahisi preshaaa sijawahi kuona mwanaume kamili kama huuyuuu " Masha alikuwa anajisemeza mwenyewe ndani ya Gari wakati anaelekea nyumbani kwake... Kabla ya kufika nyumbani kwanza alipitia sokoni akanunua mahitaji aliyoona
0 Comments