
kutoka kijijini kwetu tukuyu kisha nilihamia mbeya mjini. Ni baada ya kuuza mpunga wangu, nilipata pesa za kutosha, niliamua kwenda mjini ili nikaanze maisha yangu. Nilifika mjini, kwakuwa nilikuwa nina pesa; sikupata tabu ya kutafuta chumba. Nilibahatika kupata chumba cha bei powa katika mtaa uitwao Sai. Nililipa kodi ya miezi sita, nilinunua vifaa vyote kuanzia kitanda, godoro, vyombo na mazaga zaga mengine. Baada ya kukamilisha chumba changu, nilitulia geto nikiwaza kuhusu biashara ya kufanya. Kichwa changu kiliwaza biashara nyingi. Niliwaza kuuza vyombo vya nyumbani au kuuza nguo. Niliwaza sana sikupata jibu!! "Ila wauzaji wa nguo ni wengi sana, bora niuze
0 Comments