
nilijifungua mapacha wakike na wakiume, Elham alizidi kujaa kichwa kaka wa familia, binti yangu mkubwa tulimuita Rahma hawa wengine tuliwaita Samira na Sameer, miezi mitatu ilipita, chausiku akaja analia, nilimpokea nakumuuliza shida nini, akasema Naseer amempiga mpaka mimba yake imetoka kisa alitaka aje kunipa taarifa kuwa anamimba ya Naseer, nilishtuka nikamuuliza, kwa kujikaza kwani nyle mlikubalianaje, kwanza alishangaa kuona niko tu kawaida sijapanic, alianza ooh dada nisamehe tu ni shemeji ndo alinilazimisha... Afu sasa hivi hanitaki tena, nilichoka Ila nikajikaza, nikamwambia tu chausiku, mimi hapa cha kukusaidia kwakweli sina kwa sababu wakati mnaanza sikuwepo nyie kaelewaneni tu mimi mtanipa mwafaka
0 Comments