
Ijapokuwa huzuni kitakapopita kicheko, umasikini ukiweka kambi katika malango yako. Ama pepo la utajiri likikupitia, iwe kwa ugumba ama kwa maradhi mshukuru yeye aliye juu. Maana yeye, Anajua kwa nini anakupitisha katika hayo, hakuna jambo linalokuja kwa akili zako mwenyewe, usijikweze. *** Katika moja ya baa maarufu yenye hadhi ya nyota tano “five star” iliyokuwa imejibebea jina katika jiji la Dar es salaam, ilijulikana kwa jina la crown hotel baa hii ilikuwa maarufu sana maana ilipendwa na watu wenye hadhi kubwa, watu walioshiba ukwasi wa fedha. Kwa wale walala njaa wasingaliweza kusogeza hata pua zao maana bei ya bidhaa zake
0 Comments