
Basi baba Dorini hakuwa na jipya maana akizidi kupinga ikafika kwenye sheria anaweza kujikuta anabaki na robo ya mali zake na huku mali zenyewe sio nyingi, basi walikubaliana na makubaliano yaliyo patikana ni kwamba wauze kila kilicho cha Baba Dorini kuanzia gari, nyumba mpaka miradi yake na wagawane fedha. Basi baada ya kuuza waligawana, nusu ya fedha ikaenda kwa baba Dorini na nusu nyingine akaichukua Lissa na hapo kila mmoja akashika hamsini zake, baba Dorini akayaanza rasmi maisha ya nyumba ya kupanga huku hajui aanzie wapi wala aishie wapi. Alipoulizia mkewe alipo akaambiwa kuwa tayari alishaolewa miezi kadhaa iliyopita, hivyo
0 Comments