
By Simulizi za john 0789 824 178 1000 Bill alinipeleka mpaka nyumbani akasalimiana na wazazi wangu hakukaa sana aliaga akaondoka.. Nilielekea namimi chumbani kwangu nikaanza kuwaza ile kiss ilivokuwa tamu isingekuwa simu kuita mpaka sasa hivi bado tungekuwa tunanyonyana tu.. Wakati nawaza hayo ghafla iliingia sms kwenye simu yangu niliifungua nikakuta imetoka kwa Bill.. Aliandika tu mke wangu❤️ nikasmile kisha nikamwambia nani mke wako?. Akajibu wewe hapo Paris Binti Lorraine ❤️ ulinioa lini?? Akaniambia nakuoa hivi karibuni❤️nyiee nilisikia raha mimi.. Tulichart mimi na Bill mpaka usiku wa manane hivi ushawahi kuchart na babe wako mpaka ukiona msg yake unapata hamu??
0 Comments