
By Babie LOve Mama alinifuata chumbani akaniuliza kuna nini?? Nilitamani kumsimulia lakini mmhh naanzaje?? Nilimwambia tu hamna kitu..Bill alikuja hapa?? Nikasema hapana mi sijamuona. Mama alikuwa ananihoji huku ananichunguza aliniangalia vizuri usoni akaona alama za vidole na hapa usoni nani kakupiga?? Nikamwambia mi sijapigwa na mtu lbda kulala muda mrefu ndo maana nikapata hizo alama nyekundu usoni.. Ooo sawa mama alichunguza chunguza pale chumbani hakuona kitu akaamua kutoka ile anatoka tu Bill akapiga simu nilivoona ni namba yake nikakata simu Sikuwa hata nimeisevu hiyo namba niliamua kuiblock ili asinipigie tena😪nilivoiblock namba ya Bill alichukua simu ya mama yake akanipigia nayo..
0 Comments