
Basi haikuchukua muda sana kama muvi ya kihindi ndani ya nusu saa tu tukafika mtipesaa , nikaagana na shogile wangu mama kibonge mie huyoo kila mtu akapita njia zake Maana yeye kidogo maisha aliyawezea japo anauza supu ya mapupu🤣🤣👌,kajitahidi mwenyewe shoo wangu anakaa kwenye chumba cha afu thelethini kina umeme japo wa mawazo ila sio ligi langu mimi nipo na kachumba ka afu ishirini cha gizaaa na bado natamba mwanamke kujiamini 🤣🤣 Kama kawaida nikawa nasokota kwato naelekea nyumbani kwanguuu ,njiani watu wote walikuwa wakinitazamaaa mie naskia rahaa balaa Jamani nimenunua mcheleee kilo 15 staki wageni lakini🤣🤣,mimi sina siri jamani
0 Comments