
kama kawaida, niliamka kwa kujitahidi sana kuhakikisha sishindwi, muda wa kwenda pared ulipofika tulienda vikosi vyote, hapo tukafanya pared kisha ukaguzi ukafika, alikuwa tayari General yupo mbele kabisa, tayari kwa kufanya ukaguzi wa vikosi, alianza kukagua kikosi kimoja hadi kingine, akafika kwenye kikosi namba saba ambacho nipo mimi, alikagua mmoja mmoja hadi kufikia kwangu, aliponifikia mimi akasimama na kunitizama, kisha aliendelea na ukaguzi. Baada ya ukaguzi kukamilika, tuliruhusiwa kwenda kupata breakfast chap chap, dakika kadhaa wakati tunapata breakfast, nilijikuta nimeshika kikombe cha chai kinamoto kweli kweli hata kunywa nishida, nilipiga funda mbili tuu, kengere ikapigwa hapo hapo, ikabidi niache kunywa
0 Comments