
ENDELEA....... "Kaka mbona umezubaa!?" Oscar aliulizwa. "Nipeleke alipolazwa Belinda!" "Aya subiri mara moja!" Aliingia ndani na baada ya mda alitoka na kuufunga mlango na kuongozana na Oscar mpaka kwenye hospital aliyokuwa kalazwa Belinda aliyekuwa hoi kitandani. Urembo aliokuwa akitamba nao haukuwepo tena, Belinda alionekana kuzeeka kabra hata uzee haujamfika mpaka Oscar alimwonea huruma. "Lilly huyu ni nani!?" "Ni rafiki yake na Belinda kaja kumuona!" "Aaaaah, karibu sana kijana!" "Asante!" Oscar alijibu huku akimtazama Belinda aliyekuwa akizungumza kwa tabu na kuonesha tabasamu baada ya kumuona Oscar kafika kumtembelea na licha ya majanga aliyokuwa nayo Oscar ila aliona Belinda anamajanga zaidi yake
0 Comments