
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zuberi Homera (@juma_zuberi_homera ), ameshinda kwa kishindo kura za Maoni za Ubunge Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma kwa kuzoa ushindi katika Kata zote 21 za Jimbo hilo. Dkt. Homera ameshinda kwa kupata kura 11,836 sawa na asilimia 92%. Huku aliyekuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Vita Rashid Kawawa akiambulia kura 852. Katika kata hizo matokeo yake aliyozoa kura Dkt. Homera ni kama ifuatavyo; Lisomonji 431 Limamu 611 Mkongo nakawale 682 Mkongo Gulioni 408 Luchili 844 Luegu 468 Litola 522 Namabengo 895 Msindo 403 Mputa 282 Kitanda 543 Mgombasi 404 Likuyu 565 Rwinga 746
0 Comments