
Mtunzi: @★abuu_lion №0685086201 Baada ya kusikiliza kisa cha yule dada chote kifupi, nafsi iliniuma sana. Nilimpatia shilingi 30,000 ambayo nilikuwa nimeifanyia kibarua cha kuvuna alizeti kwa siku 4. Hivyo niliona nimpatie yule dada, kisha nikaondoka naye mpaka nyumbani kwetu. Nilimsihi asiwe na wasiwasi kwani siwezi kusema kuwa alitaka kumtupa mtoto—hiyo itakuwa siri kati ya mimi na yeye. Nyumbani naishi na bibi na babu kizaa mama, hivyo ni ukoo mkubwa na tuko wengi kidogo. Baada ya kufika nyumbani, tuliingia ndani na yule dada. Nilmkaribisha kwa tabasamu, kisha mama mzazi akanitoa nje faragha kwa ajili ya kujadili. "Hashim mwanangu, huyu binti ni
0 Comments