KATOTO KA 2000 KALIVYONIFANYA NIISAHAU NDOA YANGU----EP 01

KATOTO KA 2000 KALIVYONIFANYA NIISAHAU NDOA YANGU----EP 01

"Mambo" kalinisalimia katoto kale ambako kimuonekano umri wake na wangu haulingani kabisa yani tumeachana mbali kama ardhi na mbingu. "Ama kweli dunia imevaa skeiti wewe mtoto unamsalimia nani hivyo?😳" Nilikaambia huku nikiwa nimekatolea macho makali kabisa "Mshua acha hizo bhana mtoto nani? Mbona unakaa kama mgeni wa jiji, ulitaka nikuambie shikamoo? Hizo ni salamu za watumwa, zipo huko mikoani lakini si hapa Dar, acha ushamba" Kalinijibu majibu hayo nikabaki nimeduwaa tu huku domo langu likiwa wazi mithili ya mamba anayetega samaki baharini. Kwakweli nilishangaa sana kwani ukikaangalia katoto kale kanapatana umri na mtoto wangu wanne. Lakini hata hivyo nikayachambua majibu

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments