
Nabii Ya’qub (a.s) alitoroka Palestina kwa amri ya mama yake, aliyekuwa na hofu juu yake kwa sababu ya chuki na hasira ya ndugu yake Esau, ambaye alimchukia kutokana na urithi wa unabii kutoka kwa baba yao. Alipofika nchini Iraq, kwa mjomba wake Labani, alimwona binti mdogo wa mjomba wake aitwaye Rahel, ambaye alikuwa mrembo sana na mwenye tabia njema. Akamwomba mjomba wake amuozeshwe Rahel, lakini mjomba wake Labani akamwekea sharti: “Utachunga kondoo wangu kwa miaka saba.” Ya’qub akakubali. Miaka saba ikapita, na Nabii Ya’qub akatimiza ahadi yake. Lakini mbele ya watu, mjomba wake Labani alimletea yaaqub binti yake mkubwa Lea
0 Comments