
Nikajilazimisha nikaendelea kutenga, wakati naludi jikoni nikakutana uso kwa uso na Peter,aliniita jina dah nilijuta bola ningebaki jikoni,nilimsikiliza nikaagiza binti akaenda kumhudumia, wakati wa kutoa pesa akataka mimi ndio niende nikapokee, nijaona bola nile tu hasara sio kwenda kwa uyo mpuuzi... Alisubili wee mpaka wateja wote wakaisha, yeye kaganda tu, mimi nikaona asinitanie nikamuibukia, samahani Joy bwana YesuAsifiwe... Ukweli sikuitikia hio salamu kabisa,nilimwambia tunahitaji kufunga unaweza kulipia utupishe tufunge, muda wetu umeisha... Joy nahitaji tuongee, tulekebishe makosa, nilikukosea nimetambua naomba unisamee sawa, ikiwezekana unipe nafasi ya mwisho... Peter ivi unajisikia unachokiongea mme wa mtu kabisa, pole mimi tayali ni mke
0 Comments