
Baada ya mda kupita Dada aliyazoea maisha ya kuishi bira kuwa na mme na tuliendelea kuwasiliana mara kwa mara. Nikiwa nyumbani mimi pamoja na mzoa taka niliamua kumwambia ukweli Damian ambao sikuwahi kumwambia mtu yoyote yule na ilikuwa siri yangu peke yangu. "Damian huyu mtoto niliyenae wewe ndiye baba yake mzazi na sio Alex" nilimwambia Damian au mzoa taka. Hakuamini kile nilichomwambia zaidi ya kuniuliza kwa kile nilichokisema na mimi nilimhakikishia kuwa ni mtoto wake, tangu siku hiyo Damian alikuwa akiujua ukweli kuwa Grace ni mtoto wake. Siku mbili zilipita tangu nimweleze ukweli Damian kuhusu mwanangu Grace na siku hiyo
0 Comments