
Siku zilizidi kwenda nikiwa naendelea kuishi na mzoa taka na hakuwa tena kupatwa na tatizo la ukichaa. Siku moja nikiwa kazini Alex alinitumia ujumbe na kuniambia kuwa lazima atahakikisha kuwa mimi na Mzoa taka tunatengana na mimi kwa hasira niliamua kumpigia na bahati nzuri alipokea simu. "Ivi Alex unafikiri mimi natishika na maneno yako!?" Ilibidi nilimuulize. "Unajiamini sana Irene subiri utaona" Alex aliongea. "Basi sawa tuone kama utaweza kututenganisha" nilimjibu na baadae nilikata simu. Baada ya mda kwenda nilirudi nyumbani na Mzoa taka aliporudi nilimweleza kile alichoniambia Alex. "Kipenzi hayo ni maneno ya mkosaji tu wewe mwache asumbuke huko ila
0 Comments