
Nilishangaa kumuona Mzoa taka akibadirika gafra na kuwa kichaa kwani alitoka nje akiwa hivyo hivyo uchi. "Wewe Damian" nilimwita lakini Damian hakutaka kunisikia. Nilihisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Mzoa taka ametoka nje akiwa uchi, haraka nilienda kuvaa dela langu nakutoka kwa ajili ya kumfatilia mzoa taka. Nilifika nje nakumuona Mzoa taka akikimbia huku akiwa uchi na baadhi ya watu waliokuwa wanamwangalia walianza kumcheka baada ya kuona mtalimbo wake. Ilibidi nianze kupiga kelele kwa ajili ya kutafta msaada na bahati nzuri kulikuwa na vijana waliomuona Mzoa taka nakuanza kumkimbiza nakufanikiwa kumshika. Damian aliletwa huku akiwa anachekacheka kama mtu aliyelukwa na akili.
0 Comments