
Alex aliniona nikiwa nimeongozana na mzoa taka. "Heeeh kumbe bado hamjaachana!?" Alex alituuliza na mimi niliamua kumjibu. "Wewe ulitakaje kwani!?" "Wewe mwanamke kumbe bado unajifanya jeuri sana subiri utaona" Alex aliongea na mimi mda huo hasira zilianza kunishika hasa baada ya kukumbuka kile alichomfanyia dada yangu na kutaka kuvunja mahusiano yetu mimi na Mzoa taka kwa kumtumia Suzi. "Baada ya kumuambukiza dada yangu umeona haitoshi unataka uniambukize na mimi sindio!?" Baada ya kuongea Alex alishituka. "Kumuambukiza...!?" "Kwahiyo unajifanya hujui ulichokifanya kwa dada!?" niliongea na Alex aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka kwa speed. Mzoa taka aliniangalia na kuniuliza "Irene
0 Comments