
"Kama unataka kuvuruga maisha yangu basi fika nyumbani kwetu ili tumalizie mchezo mapema na wewe iibuke mshindi . Suzan alimaliza kuongea alafu akataka kufungua mlango lakini Victor alizuia kwa kuushika mkono wake. " Nini,Kwani bado haujamaliza kuongea? Au ndio unataka kuendelea kukaa na mimi uendelee kunitishia maisha? " Kwako huwa simalizi kuongea na wala sichoki kila muda nahisi kuna jambo jipya la kukueleza. Na kuhusu kutishia ni uwongo bali na kueleza kutoka moyoni sababu nipo tayari kufanya kile ninachofikiria. Suzan alivuta mkono wake "Niache niwahi darasani. " Sawa mpenzi ila naomba kitu kimoja kabla haujashuka kwenye gari. " sema haraka.
0 Comments