
Suzan aliingia darasani kila mtu alimuangalia , James alionekana kuwa na wasiwasi na ujio wa Victor na kulikuwa na tetesi kuwa suzan amepata mwanaume mwenye pesa anampeleka chuo na gari ya kifahari. Wakati wa mapumziko Suzan alikuwa amekaa na wenzie na mazungumzo yao yalikuwa ni kuhusu Victor. Mara James alifika . " Samahani suzan tunaweza kuongea mara moja. " Sawa. Suzan alinyanyuka wakasogea pembeni huku nyuma wakina Diana wakaanza mjadala mpya. " Huyu nae ananisumbua tu mwenzie kasapata handsome wake wa nguvu. " Lakini kweli James akalazimisha penzi na jinsi alivyokuwa na bahati kapewa kakubaliwa na muda mchache tu ananyang'anywa
0 Comments