MIMBA YA DHARURA* *SEHEMU YA SITA*

MIMBA YA DHARURA*   *SEHEMU YA SITA*

Chumba cha hospitali kilijaa ukimya mzito baada ya daktari kutoa taarifa. Maneno yale “Nadia ni mjamzito wa mwezi mmoja na wiki kadhaa” yalibaki yakining’inia hewani kama radi iliyopiga katikati ya anga. Mama yake Nadia alishika kifua chake kwa mshangao. “Eeeh Mungu wangu… Nadia, hivi ni kweli hiki nilichokisijia? Nadia alimuangalia mama yake huku machozi yakitiririsha. Baba yake alisimama akitetemeka kwa hasira “Hii aibu umetuletea kutoka wapi? Wewe ni binti wa heshima, uliyekuwa ukitazamwa na jamii nzima. Umekuwaje? Na hii mimba ni ya nani? Nadia alishindwa kujibu maswali ya baba yake alijikuta machozi yakimtoka bila kukoma. Alitamani ardhi ipasuke imfunike pale

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments